Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kampuni ya mawasiliano ya Yas na huduma yake ya kifedha ya Mixx by Yas imeandaa hafla maalum iliyowakutanisha wadau na watoa huduma wake kutoka maeneo mbalimbali. 

Hafla hiyo ililenga kujenga mshikamano, kusikilizana kwa karibu na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu namna bora ya kumhudumia mteja.

Hafla hiyo ilitumiwa pia kama fursa ya kipekee ya kuthamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na kila mshirika na mtoa huduma katika safari ya pamoja ya kuboresha uzoefu wa wateja. 

Kupitia mijadala na mazungumzo ya wazi, washiriki walipata nafasi ya kusherehekea mafanikio yaliyopatikana na kujadili changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma.