Makamu mpya wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameapishwa rasmi Jumamosi Agosti 29, 2026 katika hafla ya hadhi iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, ambapo kiapo chake kimesimamiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania George Masaju mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Ndejembi ambaye awali alikuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chamwino, ameteuliwa kushika nafasi hiyo ya pili kwa ukubwa Serikalini baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kutangaza kujiuzulu Agosti 25, 2026. 

Uteuzi wake ulipitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Agosti 26 na kupata ithibati ya Bunge kabla ya kuapishwa, ambapo katika hotuba yake ya kwanza ameahidi kufanya kazi kwa uaminifu, uzalendo na utii mkubwa kwa Rais katika kumuunga mkono kutekeleza majukumu ya Taifa. 

Hongera sana Mhe. Deogratius Ndejembi. 👏🏽