Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Gladness Kifaluka ametangaza rasmi uzinduzi wa bidhaa yake mpya ya marashi inayojulikana kama “Parfume By Daka”. 

Kupitia chapisho lililowekwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo ambaye pia hujihusisha na utayarishaji wa vipindi alieleza furaha na shukrani zake kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha hatua hiyo mpya ya kibiashara huku akionyesha paketi ya bidhaa hiyo. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika chapisho hilo, manukato hayo ya Dakaperfume yanapatikana kila kona nchini kwa bei nafuu na za kawaida sana ili kuwafikia wateja wengi. 

Tangazo hilo limevutia hisia na pongezi kutoka kwa wafuasi wake mtandaoni, likionyesha namna wasanii wanavyotumia majukwaa ya kidijitali kupanua wigo wao wa kipato na kuongeza ushindani katika soko la manukato.