Habari njema imetawala kutoka nyumbani kwa muigizaji maarufu na mkongwe nchini Tanzania, Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa, baada ya binti yake, Sonia George anayefahamika kama Sonia Monalisa, kuandika historia kwa kuhitimu Shahada ya Kwanza kwa Heshima ya Daraja la Kwanza (First Class Degree).

Mafanikio hayo yameleta furaha kubwa kwa familia, ambapo Yvonne Cherry (Monalisa) ameonyesha furaha na fahari kubwa na kujivunia juhudi, nidhamu na kujituma kwa binti yake katika kipindi chote cha masomo.

Mashabiki na wadau wamejitokeza kumpongeza Sonia kwa hatua hiyo adhimu ya kitaaluma na kumtakia mafanikio mema katika safari yake inayofuata.

Hongera sana Sonia! 👏🏽