Chapa maarufu ya mtindo ya Denim Tears, ikishirikiana na Adidas Originals, imezindua rasmi viatu vipya vilivyopewa jina la “Ghana Must Go.” Hatua hii inaadhimisha mwanzo wa mradi na ushirikiano wa miaka mingi kati ya pande hizo mbili. 

Mbunifu Tremaine Emory ametumia muundo wa mistari na mraba unaofahamika sana kwenye mifuko ya “Ghana Must Go” kubadilisha muonekano wa viatu vya Superstar 82 na Stan Smith 80. Vilevile, jozi zote mbili zina alama ya Sankofa kutoka utamaduni wa Waakan wa Ghana, yenye maana ya “rudi nyuma ukachukue.”

Viatu hivi vilivyobuniwa kwa mchanganyiko wa utamaduni na mtindo wa kisasa vinatarajiwa kuingizwa sokoni rasmi tarehe 7 Novemba 2026, ambapo vitauzwa pekee jijini New York. Kuhusu gharama zake, toleo la Superstar 82 litauzwa kwa dola 180 za Marekani (US180), wakati toleo la Stan Smith 80 itapatikana kwa dola 160 za Marekani (US160).