
Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imezindua rasmi Mtandao wa Viwango Tanzania, ikiahidi kuondoa usumbufu wa mandao kwa wateja wake kupitia mtandao ulioenea nchi nzima wenye kasi na usiokwama.
Ili kuhakikisha kila sehemu nchini inafikiwa na huduma za 4G na 5G, Yas imetangaza uwekezaji wa zaidi ya shilingi trilioni moja za Kitanzania kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Yas Tanzania, Wonde Shisael, alisema kuwa idadi kubwa ya minara waliyonayo nchi nzima pamoja na kasi ya huduma zao ndiyo sababu kuu inayowafanya leo kutambulika rasmi kama ‘Mtandao wa Viwango’.



