
Jokate Mwegelo amekuja na Kidoti Foundation akiwa na dhamira ya kufungua milango ya ubunifu kwa kizazi kijacho, na jana Aprili 29, 2026 ameanza kwa vitendo.
Ameongoza wanafunzi takribani 110 wanaosomea sayansi kutoka Shule ya Sekondari ya Jokate Mwegelo, Kisarawe, hadi STEM Park Dar es Salaam kwa mafunzo yanayochochea fikra za ubunifu katika ulimwengu huu wa kidigitali.
Hongera sana Jokate! 👏🏽











