
Mwanamitindo, mjasiriamali na mwanaharakati wa haki za wasichana, Flaviana Matata, ametangazwa rasmi kuwa 2026 OC Fellow na Opportunity Collaboration (OC).
Baada ya kumaliza chuo, Flaviana Matata alishiriki Miss Universe Tanzania 2007 na kuingia Top 10 duniani. Ingawa alifanikiwa kwenye umodelling, alikataa kuchukuliwa kama sura tu.
Alipolazimika kuchagua kati ya kuendelea na masomo au kazi ya uanamitindo, aliwaza wasichana wa Tanzania wanaokosa fursa kwa sababu ya umaskini, mila kandamizi na mifumo dhaifu.
Hali hiyo ilimfanya Flaviana kuanzisha Flaviana Matata Foundation (FMF). FMF haikomi kutoa ufadhili wa masomo pekee – inatatua changamoto za kimfumo zinazowazuia wasichana kwenda shule kama ndoa za utotoni, umaskini na ubaguzi wa kijinsia.
Kupitia ushirikiano na jamii, utetezi wa sera, familia, shule na viongozi wa kimila, FMF inajenga fursa na mazingira yanayolinda elimu ya msichana. Kwa Flaviana, “Msichana anayemaliza elimu yake anakuwa chachu ya mabadiliko kwa vizazi.”
OC Fellowship ni programu ya kimataifa inayowaleta pamoja viongozi wa kibunifu wanaopambana na umaskini na ukosefu wa haki. Washiriki wa 2026 watakutana Albufeira, Ureno kuanzia Novemba 1-6, 2026. OC inamlenga Flaviana kama kielelezo cha viongozi wanaoshughulikia chanzo cha matatizo, si dalili tu.
Hongera sana Flaviana Matata!
