April 6, 2026

Staa wa muziki wa R&B nchini Tanzania, Juma Jux, ameweka wazi hisia zake za furaha tangu alipoingia kwenye majukumu ya kulea, akieleza kuwa kuitwa “baba” kumebadilisha mtazamo wa maisha yake kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza kwa hisia kupitia kipindi cha #TheSwitch ndani ya Wasafi FM, Jux amekiri kuwa ujio wa mtoto katika maisha ya mwanadamu huleta mapinduzi ya namna unavyouchukulia ulimwengu.

Najisikia vizuri sana kuitwa baba. Mtoto anapokuja kwenye maisha yako, kila kitu kinabadilika kabisa, yaani ni amazing,” alisema Jux.

Kauli hiyo imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake ambao wamekuwa wakifuatilia maisha ya msanii huyo nje ya jukwaa. Jux anaungana na mfululizo wa mastaa wa kiume nchini ambao wamekuwa wakijivunia hadhi ya ubaba na kuonesha upande wao wa upendo na uwajibikaji kwa familia zao.