April 6, 2026

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Uongozi “Honorary Award – Excellent Leadership Icon” katika hafla ya Tuzo za East Africa Youth Awards iliyofanyika Aprili 4, 2026 Jijini Arusha.

Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Vijana na jamii, ikiwa ni matokeo ya utendaji wake uliotukuka katika nafasi mbalimbali za Uongozi Serikalini.

Jokate ni miongoni mwa Viongozi Vijana waliopitia nyanja tofauti zikiwemo Siasa, Uongozi wa umma na harakati za kijamii, akijijengea taswira ya Kiongozi mwenye maono na anayejali matokeo, hali iliyomfanya kuibuka kinara katika tuzo hizo za East Africa Youth Awards.