Amini kwamba jambo bora zaidi linakuja kwako, hata kama leo kila kitu kinaonekana kizito na giza. Maisha si mstari ulionyooka, ni safari yenye milima na mabonde, na wakati mwingine kuchelewa kwako si kukataliwa bali ni maandalizi. 

Kila machozi uliyowahi kutoa, kila dua uliyoinua usiku, kila jitihada uliyofanya kimya kimya bila mtu kukuona, vyote vina hesabiwa. Usijilinganishe na safari ya mtu mwingine, maana maua hayachanui kwa wakati mmoja. 

Endelea kupanda mbegu za wema, subira na bidii, jifunze kupumzika lakini usikate tamaa. Yale uliyoyapoteza yalikuwa fundisho, yale unayoyasubiri yatakuwa zawadi. 

Fungua moyo wako, tabasamu tena, na amini kwa dhati kwamba kesho yako itakuwa bora kuliko jana yako.