IKFIEDBUSINESS

Tatizo la wajasiriamali wengi sio kukosa wateja. Tatizo ni kuwatafuta wateja kabla ya kuwa na mahali pa kuwaweka.

Tumezoea kufanya kazi bila mpangilio. Lead zaidi, DM zaidi, simu zaidi. Ukipata wateja 5 kila kitu kinachanganyikana. Message inapotea, kazi inachelewa, ubora hauko sawa, pesa inasahaulika, unakosa usingizi, mteja anaondoka na malalamiko. Unasema biashara ni ngumu. Biashara sio ngumu. Biashara bila mfumo ndio ngumu.

Mfumo sio software ya gharama. Ni kuandika tu hatua kwa hatua kazi inavyofanyika ili iende hata usipo kuwepo. Usitafute maji kabla ya bomba. Wateja ni maji. Mfumo ni bomba.

Kabla ya kutumia hela kwenye matangazo, jenga mifumo hii mitano ya msingi:

1. Mfumo wa wateja: 

Kila lead anaingia wapi? Unamfuatiliaje? Unamkumbukaje? Kama kila kitu kiko kichwani na WhatsApp, huna biashara, una fujo.

2. Mfumo wa mauzo na onboarding: 

Mteja akisema ndio, nini kinatokea? Kuna mkataba? Invoice? Ujumbe wa kumkaribisha? Timeline ya kazi? Kama unabuni upya kila mara, utachoka.

3. Mfumo wa utoaji huduma (SOP): 

Hii ndio moyo wa biashara. Hatua ya 1, 2, 3 kutoa matokeo. Imeandikwa vizuri kiasi kwamba ukimpa mtu mwingine kesho anaweza kuifanya na matokeo ni yale yale. Hii ndio inaleta ubora.

4. Mfumo wa fedha: 

Una-track faida au mapato tu? Mshahara wako, kodi, mtaji, matumizi vimetengwa? Biashara nyingi hazifi kwa kukosa wateja, zinafia kwa kukosa mfumo wa pesa.

5. Mfumo wa masoko: 

Kila siku usiamke na swali “leo nipost nini?” Jenga kalenda ya maudhui, ujumbe wa moja kwa moja wa kufuatilia wateja, na script ya mauzo inayorudiwa.

Mfumo ukiwepo, mteja 1 na 100 ni sawa. Unaweza kuondoka wiki biashara inaendelea. Mtu mpya akiajiriwa leo, kesho anaanza kazi, mfumo unamfundisha.