Nike na chapa ya mavazi ya Kim Kardashian, SKIMS, zinatarajiwa kuleta muonekano mpya katika ulimwengu wa viatu vya michezo kupitia toleo lao jipya la viatu vya ‘NikeSKIMS Waffle Racer’.

Ushirikiano huu unaoongozwa na mjasiriamali na nyota wa mtindo wa maisha Kim Kardashian unaihuisha upya viatu maarufu vya kukimbia vya Nike vilivyobuniwa mara ya kwanza mwaka 1977, ukichanganya asili yake ya zamani na muundo wa kisasa unaoadhimisha mtindo wa urembo wa SKIMS.  

Viatu hivi vimepangwa kuzinduliwa rasmi mnamo Novemba 10, vikionyesha hatua nyingine muhimu katika kuimarisha ushirikiano unaokua kati ya chapa ya Nike na Kim Kardashian. 

Muungano huu unathibitisha kuwa pale urithi wa zamani unapokutana na mtazamo mpya wa kibunifu wa Kim Kardashian, hata kielelezo cha zamani kinaweza kuvutia kizazi kipya cha mashabiki.