
Kampuni ya Meta metangaza Jumanne kupitia tovuti yake kuwa programu ya Threads imefikia watumiaji milioni 500 wanaotumia huduma hiyo kila mwezi. Kuadhimisha hatua hiyo, Meta imezindua mfululizo wa vipengele vipya vinavyolenga kuimarisha ushirikiano wa kijamii ndani ya jukwaa.
Kulingana na taarifa ya kampuni, ukuaji huo mkubwa umechangiwa zaidi na jamii, yaani makundi ya watumiaji wanaoungana kwa maslahi yanayofanana kwenye Threads, kuanzia vitabu na mpira wa kikapu hadi malezi ya watoto na muziki.
Kutokana na mafanikio hayo, Meta inatumia hatua hii kuhitimisha awamu ya majaribio ya kipengele cha jamii na kukizindua rasmi pamoja na vipengele kadhaa vipya vitavyosaidia wasimamizi na wanachama kushirikiana kwa karibu zaidi.
