
Guinness World Records imemtambua rasmi mpishi maarufu kutoka Nigeria, kama ICON, akipongezwa kwa ushawishi na uvumilivu wake uliohamasisha kizazi kipya barani Afrika.
Hilda Bassey, mzaliwa wa Jimbo la Akwa Ibom, alianza kupika akiwa na umri wa miaka mitano tu akimsaidia mama yake mgahawani, shauku ambayo baadaye ilivutia ulimwengu.

Mwaka 2023 alitikisa mitandao ya kijamii baada ya kuvunja rekodi ya kupika mfululizo kwa muda mrefu zaidi kama mtu binafsi, akipika bila kusimama kwa saa 93 na dakika 11 huku akiandaa mapishi 55 na kuzidi rekodi ya awali ya Lata Tondon.
Ingawa mpishi Alan Fisher kutoka Ireland aliivunja rekodi hiyo baadaye, Hilda aliendelea kung’ara na mwaka 2025 akaweka rekodi nyingine ya Guinness kwa kuandaa wali wa kukaanga mtindo wa Nigeria kwa wingi mkubwa zaidi kuwahi kutokea.
Kwa sasa Guinness World Records inamheshimu si kwa mafanikio yake tu, bali pia kwa uthabiti, ushawishi wake, na fahari anayoiwakilisha kwa mamilioni barani Africa na duniani kote, akiwa miongoni mwa ICONS wanaoadhimisha watu na matukio yanayounda dunia yetu.
Hongera sana Hilda Baci! 👏🏽
