IkFiedBliss

Kuna nyakati maisha milango inafungwa, mipango inabadilika na moyo unauliza kama umesahaulika, lakini ukweli ni kwamba haujawahi kupotea. 

Kila kushindwa kulikuwa kukikuelekeza upya, na kila kipindi cha ukimya kilikuwa kinakujenga uwe tayari kubeba baraka ulizoziomba, kwa sababu kimya kimya kila kitu kinapangika kwa ajili yako. 

Hakuna kilichopotea bure, hata machozi na kusubiri vyote vilikuwa vinaunganishwa kwa hekima kukutengenezea kesho iliyo bora kuliko jana. 

Usikate tamaa na endelea kusonga mbele kwa moyo mpole, kile kilichoandikwa kwa ajili yako tayari kinakuja na siku moja utaelewa kwa nini ilibidi kila kitu kitokee hivyo.