
Idris Sultan amechaguliwa ku-host Tuzo kubwa zaidi za vijana Africa, The Future Awards Africa (TFAA) kwa toleo lao la miaka 20.
Mwaka huu TFAA inafanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika, kukusanya nyota watano kutoka pembe tano za Africa.

Idris ataiwakilisha Tanzania, akishirikiana na staa wa Nigeria Genoveva Umeh, mtangazaji mahiri wa Malawi Priscilla Kayira, Resego Motlhokathari kutoka Botswana na Claudia Nasibwa wa Kenya.
Usiku huo wa kihistoria utang’aa Novemba hii ndani ya Balmoral Events Centre, Lagos, Nigeria chini ya theme ya “Africa’s AI Generation” – kuenzi vijana wanaotumia akili bandia na ubunifu kuiongoza Africa ya kesho.
Hongera sana Idris! 👏🏽
