Mjasiriamali kijana kutoka Tanzania, Leodger L. Kachebonaho, ameandikisha historia baada ya kutajwa miongoni mwa vijana 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika kwa mwaka huu. Tuzo hizo zilitolewa na Pan-African Youth Foundation jijini Accra, Ghana, zikiwalenga vijana walioonyesha ubunifu, uongozi na mchango mkubwa katika kubadilisha jamii zao. 

Leodger anafahamika kwa ari yake ya kujitolea kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii, huku akisimamia kwa mafanikio kampuni ya KPD Clearing and Forwarding na Emwani Coffee Limited. Biashara zake zimekuwa chachu ya ajira kwa vijana wengi na zimechangia kukuza taswira ya bidhaa za Kitanzania katika soko la kimataifa.

Mbali na kuwa mfanyabiashara, Leodger amejitolea kujenga taasisi imara zinazowajenga uwezo wananchi na kuimarisha maendeleo jumuishi. Anawakilisha kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika wanaogeuza changamoto kuwa fursa na kuhakikisha kuwa uthabiti wa kibiashara unatafsiriwa kuwa manufaa ya moja kwa moja kwa jamii. 

Hongera sana Leodger! 👏🏽