Benki ya UBA Tanzania imeendelea kuweka dhana ya utunzaji wa mazingira katika vitendo kupitia Mpango wa Uendelevu wa Kundi la UBA, uliolenga kukuza siku zijazo zenye ukijani na uendelevu zaidi. 

Katika kuitikia wito wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Dora Kyungu, wafanyikazi wa UBA Tanzania wamepatiwa miche ya miti kama ukumbusho wa jukumu la kila mtu katika kulinda na kutunza mazingira yanayomzunguka.

Hatua hii inadhihirisha dhamira ya benki hiyo kwamba utunzaji wa mazingira ni zaidi ya maneno, bali ni kuchukua hatua madhubuti zitakazohamasisha mabadiliko chanya kwenye jamii. 

Kupitia utunzaji wa miti hiyo, UBA Tanzania inawekeza katika mustakabali ambapo jamii na mazingira vinafanikiwa kwa pamoja, ikiongozwa na kaulimbiu yao ya “Benki Moja. Sayari Moja. Jukumu Moja.”