
Mwimbaji na mfanyabiashara maarufu Vanessa Mdee ametangaza rasmi kuanza kwa sura mpya ya maisha yake ya kibiashara baada ya kuzindua brand ya bidhaa za urembo inayoitwa Cash Madame.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa Mdee amewashukuru mashabiki zake kwa kuwa naye tangu mwanzo wa safari yake na kuwakaribisha kujipatia bidhaa hizo mpya, zikianza na mafuta ya lips (lip balms).
“Mmenishuhudia nikikua. Sasa, karibuni kwenye awamu yangu mpya. CASH MADAME imefunguliwa rasmi. Nunua mafuta yetu ya lips kupitia kiunganishi (link) kilichopo kwenye bio yangu: www.cashmadame.com,” aliandika Vanessa.
Kwa wakazi wa Afrika Mashariki, mwanamuziki huyo amebainisha kuwa bidhaa hizo zitapatikana kwa upekee kupitia maduka ya Zurii House of Beauty. Mashabiki na wateja wanaweza pia kutembelea tovuti rasmi ya biashara hiyo ili kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.
Hongera sana Vanessa! 👏🏽



