IkFiedNow

Kila himaya huanza na wakati mdogo wa ujasiri. Kwa Willy the Tailor, muasisi na Mkurugenzi Mbunifu wa William Taylor, wakati huo ulikuwa ni uwasilishaji wa darasani chuoni. Hakuwa na suti ya bei ghali, alichokuwa nacho ni maono. Akachukua koti hapa, suruali pale, akaviunganisha kwa mtindo wake mwenyewe.

Watu wakagundua. Marafiki wakapenda kile alichokuwa amevaa, wakaanza kumuuliza “bro, nitapata wapi hii?” Ndipo alipogundua kuwa mavazi ni zaidi ya nguo tu, ni lugha. Baada ya kumaliza chuo, wakati wengine walienda kutafuta kazi, yeye aliamua kutengeneza kazi. Lengo lake lilikuwa rahisi lakini lina uzito: alitaka kuongeza mwanga, hata best man kwenye harusi na yeye pia apate kuonekana. Kutoka kwenye ndoto hiyo, mwaka 2018, William Taylor ilizaliwa Dar es Salaam.

Falsafa yake tangu siku ya kwanza imekuwa wazi: Afrika Mashariki inastahili chapa ya mavazi ya kifahari ya kiume inayozungumza kutokana na uzoefu wake wenyewe – sio ya kuazima kutoka kwenye mapokeo ya Ulaya, bali iliyo katika mazungumzo ya kweli nayo. Huu ndio ustahimilivu uliomfanya asimame. Kujenga chapa ya kifahari kutoka sifuri kwenye soko lililozoea kuagiza kila kitu kutoka nje, si rahisi.

Lakini kwa ufundi wa Kitanzania uliochanganyika na umahiri wa kimataifa, Willy aliijenga taratibu. Kutoka suti moja hadi wateja zaidi ya 800 wa nguo zilizoshonwa mahsusi, na kutoka atelier ndogo ya Dar hadi kuonyesha kazi zake Johannesburg – Afrika Kusini mwaka 2023, kila mshono umekuwa ni uthibitisho wa ubora. Kila kipande kimetengenezwa kwenda na mwanaume wa kisasa – kutoka ukumbini hadi fukwe za bahari, kutoka atelier hadi ulimwenguni.

Na sasa, sura mpya imefunguliwa. Kama ulimjua William Taylor kama Nyumba ya Suti, ni wakati wa kumjua upya kama Nyumba ya Mtindo wa Maisha. Chapa imekua zaidi ya suti zilizoshonwa mahsusi. Kuna nyongeza mpya: Viatu, Mashati ya Linen, Suruali za Linen, Suruali za Mbunifu, Polo za William Taylor, T-shirt za kawaida, Kofia, Vifaa vya ziada, Mifuko ya Tote, na kwa mara ya kwanza kabisa, Mikoba ya Wanawake na Mavazi Kamili ya Wanawake.

Ni upanuzi unaosema, sasa tunamvaa kila mtu. Na upanuzi huu una nyumba yake rasmi – mwaka huu wamefungua duka lao kuu la flagship katika Dar Village Mall, Dar es Salaam. Hii si duka tu, ni sherehe ya safari ya miaka saba ya ustahimilivu, ubunifu na ubora.