IkFiedBliss

Watu wengi hupoteza ndoto zao si kwa sababu hawana uwezo, bali kwa sababu wanasubiri wakati sahihi ambao haujawahi kuja.
Kujaribu ndiko kunakofungua milango ambayo hofu ilikuwa imeifunga, ndiko darasa halisi la maisha ambapo hata ukianguka unajifunza, hata ukishindwa unasonga mbele.
Kila kovu lina somo, kila jaribio lina nguvu inayokujenga upya kuwa jasiri zaidi. Usikubali ndoto zako zife kimya moyoni kwa kelele za mashaka ya watu au sauti ya ndani inayokuambia huwezi.
Dunia inawaheshimu wanaothubutu, na baraka hufuata juhudi, kwa sababu ndani ya kujaribu mnaishi matumaini.
