
Mwanamitindo na mfanyabiashara mashuhuri, Jordyn Woods, ameeleza furaha na shukrani zake kubwa baada ya kutunukiwa tuzo ya Power Rising na jarida maarufu la Forbes. Tuzo hiyo imekuja ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu alipozindua upya chapa yake ya mavazi ya Woods By Jordyn.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jordyn ameshiriki hisia zake kuhusu safari hiyo na changamoto za nyuma ya pazia zilizofanikisha mafanikio hayo:
“Imekuwa mwaka wa aina gani huu! Kutambuliwa na Forbes kwa Tuzo ya Power Rising katika mwaka wa kwanza tu wa kuzindua upya @woodsbyjordyn ni heshima kubwa sana kwangu. Mwaka huu uliopita umekuwa wa kuamini maono yangu, kujiamini mimi mwenyewe, na kujenga kitu ambacho ni changu halisi,” aliandika Jordyn.
Ameongeza kuwa kuna mambo mengi yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo watu hawayaoni, lakini nyakati kama hizi humkumbusha kuwa kazi ngumu, hatari anazochukua, na kujitolea kwake yote ni sehemu ya jambo kubwa zaidi.
Hongera Sana Jordyn! 👏🏽
