Mshambuliaji mahiri wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza, Bukayo Saka, ametunukiwa Tuzo ya Sócrates katika hafla ya Ballon d’Or 2026 iliyofanyika katika Ukumbi wa Palladium jijini London. 

Tuzo hiyo mashuhuri, ambayo hutolewa maalum kuwaenzi wachezaji wanaotumia ushawishi wao kuleta mabadiliko chanya ya kibinadamu duniani, imemwangazia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutokana na moyo wake wa kujitolea na kujali jamii.

Mchango mkubwa wa Saka umezalisha matunda kupitia ushirikiano wake na shirika la kutoa misaada la BigShoe, ambapo amefadhili upasuaji wa kuokoa maisha kwa zaidi ya watoto 120 jijini Kano, Nigeria. Msaada huo umewawezesha watoto wanaosumbuliwa na matatizo makubwa ya kiafya- ikiwemo ngiri na matatizo ya ubongo – kupata matibabu ya kitalamu. 

Aidha, juhudi zake zimeenea katika maeneo mengine barani Afrika kwa kufadhili upasuaji wa macho ili kurejesha uwezo wa kuona kwa watoto wenye uhitaji.

Mwanasoka huyo, aliyezaliwa London na wazazi wenye asili ya Nigeria, alikabidhiwa kombe hilo la heshima na mwanamuziki nguli wa Nigeria na mshindi wa Tuzo za Grammy, Burna Boy, katika tukio lililokutanisha mastaa hao wawili wenye mizizi mamoja. 

Akionyesha shukrani zake kupitia mitandao ya kijamii baada ya hafla hiyo, Saka alieleza kuwa anajivunia hatua zote alizopiga uwanjani na nje ya uwanja, huku akiahidi kuendelea kutumia nafasi yake kubadilisha maisha ya wengine.

Hongera sana Bukayo! 👏🏽