IKFIED BLISS

Mafanikio makubwa huwa ni matokeo ya juhudi ndogo zinazofanyika kwa mwendelezo, sio miujiza ya siku moja. Watu wengi wanakwama wakisubiri wakati sahihi, pesa nyingi au nguvu kubwa ndipo waanze kutimiza ndoto zao, kumbe siri iko katika kuanza na kidogo ulichonacho leo. 

Ukijizoeza kusoma kidogo, kuwekeza kidogo, kufanya mazoezi kwa dakika chache na kuboresha tabia moja kila siku, akili yako na mwili wako hujenga nidhamu ambayo baadaye inakuwa nguvu kubwa. 

Usipuuze nguvu ya hatua ndogo kwa sababu ndizo zinazokuondolea uvivu, zinazokupa ujasiri na zinazokufanya usonge mbele hata siku unapokosa motisha, na mwisho wa siku utagundua kuwa umbali mrefu ulioutaka umefikika kwa hatua hizo hizo ndogo.