Vijana watatu wa Kitanzania wametajwa katika orodha ya heshima ya Forbes Africa 30 Under 30 ya mwaka 2026, hatua inayotafsiriwa kama mafanikio makubwa kwa taifa kwenye jukwaa la kimataifa.

Waliotambuliwa ni Cyprian Makongoro, mwanzilishi wa Tibalabs, ambaye anatumia akili mnemba kuchambua vipimo vya umeme wa moyo na kuwezesha utambuzi wa mapema wa magonjwa hata mgonjwa akiwa nyumbani. 

Hussein Dewji wa Fair Deal Furniture amepewa heshima kwa kujenga chapa ya samani za Kitanzania zinazoshindana kikanda. huku Rosemary Raymond Kimaro wa Dianarose Logistics akitambuliwa kwa kukuza mtandao wa usafirishaji ulioenea Afrika Mashariki.

Uteuzi wa vijana hawa unaithibitishia dunia kuwa Tanzania inaendelea kuzalisha wabunifu na viongozi wa biashara wanaoleta mabadiliko makubwa barani Africa. 

Hongera sana Cyprian Makongoro, Rosemary Kimaro na Hussein Dewji!