IkFiedBliss

Hata hatua za kimya kimya bado ni maendeleo. Tumezoea kufikiri maendeleo lazima yawe makubwa, yawe na kelele na yaonekane na kila mtu, kumbe maendeleo ya kweli mara nyingi hutokea kimya kimya pasipo kushangiliwa. 

Ni ile kuamka asubuhi licha ya uchovu, kusoma ukurasa mmoja, kuacha tabia moja inayokurudisha nyuma, kuweka akiba ndogo, au kujifunza kitu kipya wakati hakuna anayekuona. Hatua hizi hazileti makofi wala hazileti likes, lakini ndizo zinazojenga msingi imara wa kesho yako. 

Usidharau mwendo wako wa pole na usijilinganishe na kasi ya wengine, kwa sababu mwendo wa taratibu unaoendelea ni bora kuliko mbio zinazokatishwa njiani, na hata ukisonga sentimita moja kila siku bado ni kusonga mbele.