BUSINESS INSIGHTS

Wajasiriamali wengi tunadhani ili biashara ikue lazima tufanye vitu vingi zaidi. Wateja wengi zaidi, masaa mengi zaidi, bidhaa nyingi zaidi. Matokeo yake tunajaza siku na shughuli ndogo ndogo na tunajisahau kuhoji kama tunasogea kweli. Kufanya zaidi bila mwelekeo ni kuchoka tu, sio kukua. Biashara nyingi hazifi kwa sababu ya uvivu, zinakufa kwa sababu ya fujo.
Biashara yako itakua pale utakapoipa nafasi ya kupumua. Unapopata nafasi ya kufikiri vizuri, ndipo unaona ukweli. Unaona ni wateja gani wanakupa hasara, ni kazi gani unapaswa kuacha, na ni fursa gani kubwa ulikuwa unaikosa kwa sababu ulikuwa bize na vitu vidogo. Maamuzi makubwa ya biashara hayaji wakati kelele ni nyingi, yanakuja wakati akili imetulia.
Usiongeze tu kazi kwenye ratiba yako, tengeneza nafasi. Kataa dili ndogo inayokupotezea mwelekeo, weka mifumo inayofanya kazi hata kama haupo, na chukulia muda wa kutafakari kama sehemu ya kazi yako. Ukuaji wa kudumu hautokani na jinsi ulivyochoka leo, unatokana na jinsi ulivyofikiri vizuri jana.
