IKFIED BLISS

Kuna nyakati maisha yanakupa hisia kwamba kila kitu kimesimama, milango imefungwa na juhudi zako hazionekani kuzaa matunda, lakini hicho unachokiita kukwama kumbe ni maandalizi ya kimya kimya. 

Ni kipindi ambacho unafundishwa subira, akili yako inapata hekima, na unajengwa kuwa imara zaidi ili isianguke inapokabidhiwa kile kikubwa unachokiomba. 

Hakuna kilichopotea, hata machozi na kusubiri kwako kuna hesabu, na siku moja utaelewa kwa nini ilibidi upitie njia hiyo ngumu. Endelea kusimama imara, jifunze, jiboreshe, na usikate tamaa, kwa sababu kile kinachokuja mbele ni kikubwa kuliko ulichopoteza nyuma.