
Leo Alhamisi, mamilioni ya watu duniani kote watakuwa wameelekeza macho yao katika tukio moja tu: sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia FIFA 2026.
Kwa kipindi cha wiki tano zijazo, soka litatawala runinga, mitandao ya kijamii, vikundi vya WhatsApp, vituo vya kuangalia mechi na sebule za nyumbani huku mataifa 48 yakimenyana nchini Canada, Mexico, na Marekani.
Hili litakuwa Kombe la Dunia kubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia, likileta pamoja timu 48 kwa mara ya kwanza badala ya 32 kama ilivyokuwa awali. Michuano hiyo itachezwa katika miji 16 iliyosambaa katika nchi tatu, ikifanya kuwa Kombe la Dunia la kwanza kuandaliwa kwa ushirikiano wa mataifa zaidi ya moja.
Mashabiki duniani kote wanatarajiwa kujumuika kutazama kila pasi, bao na shangwe zitakazoamua bingwa mpya wa dunia.
