
Benki ya NMB inaendelea kushiriki kikamilifu katika Mkutano wa Madini na Uwekezaji Tanzania (Tanzania Mining and Investment Conference 2026) unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kukuza sekta ya madini na kuchagiza uchumi wa Taifa.

Katika mkutano huo, banda la benki hiyo lilipata heshima ya kutembelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, aliyepokelewa na Mkuu wa Idara ya Miamala wa NMB, Linda Teggisa, na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu masuluhisho na fursa za kifedha zinazotolewa kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na wadau wengine katika mnyororo mzima wa thamani wa madini.

Kupitia taarifa yake, Benki ya NMB imeeleza kuwa dhamira yake kuu ni kuendelea kuimarisha upatikanaji wa mitaji, kuchochea uwekezaji na kuwawezesha wadau wa sekta hiyo kukuza biashara zao ili kuongeza mchango wa madini katika pato la Taifa. Aidha, benki hiyo imewakaribisha washiriki wa mkutano huo na wananchi kwa ujumla kutembelea banda lake lililopo JNICC ili kujifahamisha zaidi kuhusu huduma na fursa mbalimbali za kifedha zilizopo kwa ajili yao.
