Peace Hyde kutoka Ghana ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimkakati wa Kimataifa wa Time Africa, akileta uzoefu wa zaidi ya muongo mmoja katika sekta ya habari, ushirikiano na burudani. 

Hyde anaingia katika wadhifa huo baada ya kutumikia kwa zaidi ya miaka 10 katika Forbes Africa kama Mkuu wa Kitengo cha Habari za Kidijitali na Ushirikiano na Mwandishi wa Afrika Magharibi, ambapo alijikita katika kujenga ushirikiano wa kimataifa na kusimamia utayarishaji wa kazi kubwa za Kiafrika. 

Katika nafasi yake mpya, atajikita katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa Time Africa na kubaini fursa mpya, ikiwemo kuendeleza kazi asili (original intellectual property) zitakazovutia hadhira barani Africa na nje ya bara hilo.

Hongera sana Peace! 👏🏽