Chidi Blyden ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kituo cha Masomo ya Kiafrica cha Chuo Kikuu cha Harvard. Uteuzi huu umetangazwa kama hatua ya kimkakati ya kuimarisha nafasi ya kituo hicho katika kukuza utafiti, elimu na ushirikiano kati ya Marekani na Africa.

Blyden anatajwa kwa uzoefu wake mpana serikalini na sekta binafsi. Amewahi kuhudumu katika nafasi za juu ndani ya Pentagon kama Naibu Msaidizi wa Waziri wa Ulinzi anayeshughulikia Masuala ya Afrika, na baadaye kama Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Millennium Challenge Corporation (MCC) la Marekani, alikoshughulikia usimamizi wa fedha nyingi na miradi ya ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama na mataifa 53 ya Africa.

Nje ya serikali, kupitia kampuni yake binafsi ya Culturally Bound Consulting, Blyden amekuwa akijenga madaraja ya kitamaduni yanayounganisha bara la Africa na diaspora yake duniani. Kazi yake imelenga kukuza uelewa wa pamoja, uwekezaji na kubadilishana maarifa.

Akizungumzia nafasi yake mpya, Blyden ameeleza kuwa anaitazama Harvard kama jukwaa muhimu la kuisaidia dunia kuitambua Africa ya leo yenye vipaji, ubunifu na nguvu ya watu wake, na si hadithi za zamani. Ameahidi kutumia uzoefu na mitandao yake kuongeza sauti na ushawishi wa Africa katika kipindi hiki ambacho bara linazidi kuwa na mchango mkubwa katika masuala ya dunia.

Hongera sana Chidi! 👏🏽