Kipindi maarufu cha podcast cha mwigizaji na mtayarishaji maarufu wa Marekani, Keke Palmer, kiitwacho Baby, This is Keke Palmer, kimetangazwa rasmi kuwa Kipindi Bora cha Mwaka 2026 na mtandao wa Apple Podcasts. 

Ushindi huu ni uthibitisho wa bidii ya Keke Palmer, ambaye pamoja na majukumu yake ya uigizaji, utayarishaji na malezi, ameendelea kutenga muda kuandaa vipindi vyenye mafunzo makubwa kwa wasikilizaji duniani kote.

Uwezo wa kipekee wa Keke Palmer katika kuendesha mahojiano ya kina na ya wazi na watu mashuhuri kama Oprah Winfrey na Michelle Obama- ukichanganyika na ucheshi wake wa asili – ndio uliomwezesha kushinda tuzo hii kubwa ya podcast.

Hongera sana KeKe! 👏🏽