
Najua kuna siku unaamka ukiwa umechoka kabisa, hata kabla ya siku kuanza. Mambo hayakwenda kama ulivyopanga, simu yako iko kimya, na unajiuliza kama kweli kitu kizuri kitawahi kukupata wewe.
Ni sawa kujisikia hivyo. Lakini sikuzote amini jambo zuri linakaribia kutokea. Si kwa sababu maisha ni mepesi, bali kwa sababu umeshavuka mengi ambayo ulidhani yata kumaliza, na bado upo hapa.
Endelea tu kusukuma, hata kama ni hatua ndogo leo. Tabasamu lile, maombi yale ya kimya kimya, bidii ile ambayo hakuna anayoiona, vyote vinahesabika.
Usikate tamaa, jambo lako zuri lipo njiani, na labda ndiyo hili linalokaribia kugonga mlango wako.
