Si kila mpango ukivunjika ni mwisho, wakati mwingine ni mwanzo wa kweli. Hatima hukuruhusu upoteze kile ulichokidhani ni ndoto yako, ili upate nafasi ya kugundua kile ambacho kweli uliumbwa kukifanya. 

Usililie sana milango iliyofungwa, maana milango hiyo hiyo ndiyo inakuelekeza kwenye mlango sahihi. 

Maumivu ya leo, kucheleweshwa kwa leo, na kupoteza kwa leo, ni darasa linalokuandaa kuwa mtu utakayehitajika kuwa kesho.