
Mfanyabiashara na mfadhili maarufu duniani Bill Gates yupo nchini Rwanda kwa ziara maalum ya kujifunza kutokana na maendeleo ya ajabu ya nchi hiyo katika sekta ya afya. Gates ameelezea mageuzi ya mfumo wa afya wa Rwanda katika kipindi cha miaka 25 iliyopita kama moja ya hadithi za mafanikio zinazong’aa zaidi barani Afrika.
Ziara yake inajiri wakati ambapo Taasisi ya Bill & Melinda Gates, kwa ushirikiano na kampuni ya OpenAI, inaunga mkono mpango kabambe wa Dola Milioni 50 ujulikanao kama Horizon 1000 Initiative. Mpango huu unalenga kuleta mapinduzi ya teknolojia kwa kuingiza mifumo ya Akili Bandia (AI) katika zahanati na vituo vya afya kote nchini humo.
Kupitia mpango huo, wahudumu wa afya wa mstari wa mbele watawezeshwa kuboresha utambuzi wa magonjwa, kuimarisha ugawaji wa rasilimali muhimu na kuongeza ufanisi katika kufanya maamuzi, hatua itakayochangia kuimarisha zaidi mfumo wa afya wa Rwanda.
