
Si lazima uelewe kila kitu leo. Tunajilazimisha kutafuta majibu ya kila maumivu, sababu ya kila kuchelewa, na hatima ya kila ndoto iliyosimama. Kumbe kwa kutaka kuelewa kila kitu kwa haraka, tunajichosha wenyewe bila kujua.
Lakini vipi kama amani haipo kwenye kuelewa, bali kwenye kuachilia? Vipi kama siku nyingine kazi yako si kutatua, bali kupumzika tu? Ruhusu maswali mengine yabaki bila majibu kwa leo.
Ruhusu maisha yajieleze kwa muda wake. Ukiacha kujikimbiza, utagundua amani ilikuwa hapo tu, inakungoja usimame. Si udhaifu kukubali kutokujua, ni hekima. Ni namna ya kujipenda bila masharti.
Na kesho, majibu yatakuja yenyewe, taratibu, kama mwanga wa asubuhi. Leo, chagua amani kuliko presha ya kuelewa kila kitu.
