Real Madrid wamethibitisha rasmi kukamilisha usajili wa winga chipukizi wa Ivory Coast, Yan Diomandé mwenye umri wa miaka 19, akitokea RB Leipzig. Kijana huyo ameweka wino kwenye mkataba wa miaka saba utakaomuweka Santiago Bernabéu hadi Juni 2033.

Kwa mujibu wa taarifa za klabu, Madrid watalipa ada ya awali ya Euro milioni 125 na nyongeza ya milioni 15, na kufanya jumla ya milioni 140. Dau hilo linamfanya Diomandé kuwa mchezaji ghali zaidi wa Kiafrika katika historia na pia miongoni mwa usajili ghali zaidi kuwahi kufanywa na Real Madrid.

Diomandé amepanda kwa kasi ya ajabu ndani ya miaka miwili, kutoka akademi nchini Marekani hadi Leganés na kung’ara Bundesliga na Kombe la Dunia 2026 akiwa na Leipzig. Licha ya PSG kumwania kwa nguvu, ameamua kujiunga na Madrid ambapo sasa atafanya kazi chini ya kocha mpya José Mourinho akiwa pamoja na nyota Kylian Mbappé na Vinícius Júnior.

Hongera sana Yan! 👏🏽