IKFIEDBUSINESS

Tunaishi kwenye zama ambapo taarifa imezidi. Vitabu vipo, podcast zimejaa kila kona, kozi za mtandaoni ni elfu kwa elfu. Unaweza kujifunza mauzo, masoko, na uongozi ndani ya siku moja tu.
Lakini licha ya wingi huu wa maarifa, biashara nyingi hazibadiliki. Tatizo si uhaba wa elimu, tatizo ni kwamba taarifa peke yake haileti mabadiliko. Unaweza kujua kila kitu kuhusu biashara na bado ukabaki pale pale, kwa sababu mabadiliko hayatokani na kujua zaidi, yanatokana na kufanya zaidi.
Kinacholeta matokeo ya kweli kwenye biashara yako si kitabu kingine, bali ni mfumo wa uwajibikaji uliopangwa na jamii inayokulazimisha kutekeleza.
Unahitaji watu watakaokuuliza kila wiki umetekeleza nini, walio tayari kukuonyesha mapungufu yako kwa ukweli mtupu, na mazingira ambapo kutotekeleza si chaguo.
Biashara haikui kwa sababu umesikiliza podcast nzuri peke yako, inakua kwa sababu kuna mtu anakuwajibisha, kuna jamii inakusukuma, na kuna mfumo unaokufanya ufanye kazi hata siku ambazo huna motisha.
