IKFIEDBLISS

Kila kitu kinatokea kwa sababu na kwa wakati wake. Kufeli kwako leo si mwisho, ni somo. Kusubiri kwako leo kunakufundisha kuwa imara. Milango iliyofungwa, watu uliokutana nao, hata maumivu uliyopitia, vyote vina maana yake.

Usikimbilie na usijilinganishe na mtu mwingine. Maua hayachanui kwa wakati mmoja. Kila mtu ana majira yake. Fanya kazi yako kila siku kidogo kidogo, kwa imani na kwa moyo.

Usiache kuamini. Siku moja ukiangalia nyuma utaelewa kwa nini ilibidi upitie yote hayo. Utaona jinsi kila kipande kidogo cha maisha yako kilivyounganika kutengeneza picha nzuri uliyokuwa unaisubiri.