BUSINESS INSIGHTS

Biashara nyingi hazifi kwa kukosa mtaji, bali hufa kwa kukosa mwelekeo. Mwelekeo siyo tu kuwa na wazo la biashara, ni kujua kwa usahihi unakwenda wapi, unamhudumia nani, na kwa nini wewe na siyo mwingine.
Bila mwelekeo, kila fursa inaonekana kama fursa yako, na hapo ndipo unaanza kutawanyika – leo unauza nguo, kesho unajaribu chakula.
Mwelekeo unakupa nidhamu ya kusema HAPANA kwa vitu vizuri ili uweze kusema NDIO kwa kitu kimoja kizuri zaidi. Ndiyo kamba inayofunga rasilimali zako ndogo – muda, pesa, na nguvu – mahali pamoja ili zilete matokeo makubwa.
Biashara yenye mwelekeo hukua kwa sababu inajenga uaminifu na utaalamu. Unapoeleweka kwa jambo moja, wateja wanakumbuka, wanakuamini, na wanakurudia.
Mwelekeo pia unarahisisha maamuzi yote magumu: ni bidhaa gani niongeze? Ni mteja gani nimkatae? Ni tangazo gani lilipie? Jibu linatoka kwenye swali moja tu – je, hiki kinanisogeza karibu na nilipoelekea?
Biashara isiyo na mwelekeo inafanya kazi kwa bidii, lakini biashara yenye mwelekeo inafanya kazi kwa akili. Na katika soko la leo lililojaa kelele, siyo yule anayepiga kelele zaidi ndiye anayeshinda, bali ni yule ambaye ujumbe wake uko wazi, thabiti, na unaelekea sehemu moja.
