Ukuaji si mzuri tu kama unavyonekana kwenye picha za mtandaoni. Mara nyingi unaonekana kama kama Ni kurudia kitu kimoja mara kumi hadi uelewe, ni aibu ya kujaribu biashara ikafa. Ni kuamka na hofu lakini bado unaenda kazini. Hiyo ndiyo sura halisi ya ukuaji. Haipendezi, lakini ni ya kweli.

Lakini ndani ya uchovu huo ndipo unajijenga. Kila siku unapoamua kuendelea hata kama umechoka, unapanda mbegu ndani yako. Hata kama hakuna anayekuona, moyo wako unakumbuka juhudi zako. Ukuaji si haraka, ni kama mmea. Kwanza mizizi inashuka chini gizani, hakuna anayeiona. Baadaye ndipo majani yanatokea. Usijilinganishe na watu mtandaoni wanaonesha matunda tu. 

Heshimu safari yako ya kimya. Endelea kidogo kidogo. Siku moja watu watasema “ana bahati”, watasema “alipata tu”. Lakini wewe utajua ukweli. Utajua ni usiku wa machozi, ni maamuzi magumu, ni subira nyingi. 

Na hapo ndipo utasimama imara, kwa sababu msingi wako ulijengwa wakati hakuna aliyekuwa anatazama.